29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Watalii waongezeka Kilwa

Na Mwandishi wetu, Kilwa

Idadi ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani imezidi kuongezeka katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kutokana na utalii wa kihistoria na kiutamaduni.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA ),taasisi yenye dhamana ya usimamizi wa hifadhi hiyo, Februari 15, 2024 ilipokea kundi la tani la watalii 119 kutoka ikiwa ni mfululizo wa safari za watalii wa nje kutembelea hifadhi hiyo kwa shughuli za utalii.

Watalii waliowasili ni kutoka katika nchi za Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ubelgiji, Hispania na Canada wakisafirishwa na meli iitwayo Le Bougainville.

Kwa mujibu wa TAWA, hayo ni matokeo ya hatua za makusudi zilizofanywa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha sekta ya utalii nchini inakua kwa kasi baada ya kucheza filamu maarufu iitwayo Tanzania The Royal Tour.

Pia jitihada za dhati zilizofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mamlaka hiyo kwa kuboresha miundombinu wezeshi ya utalii katika hifadhi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles