OTTAWA, Canada
Â
VIONGOZI wawili wa dini   Canada wamepatikana na hatia ya kuoa wake wengi na kufungwa jela miaka mitano kila moja.
Kwa mujibu ya mahakama ya nchini Canada inasema Winston Blackmore (61) alioa wanawake 24 na mkwe wake, James Oler aliyeoa wanawake watano.
Viongozi hao wawili walipatikana na hatia ya shtaka moja la kuwaoa wanawake wengi na kila mmoja anakabiliawa na kifungo cha miaka mitano jela.
Hukumu hiyo imetajwa kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa dini   Canada.
Wote hao walikuwa ni makasisi wa dhehebu lililojitenga kutoka kanisa la Fundamentalist Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints (FLDS)
Blackmore alifukuzwa   FLDS mwaka 2002 na nafasi yake ikachukuliwa na Oler.
Matawi ya dhehebu hilo yako   Marekani ambako kuna wanachama karibu 10,000
Kuoa wanawake wengi ni kosa chini ya sheria za Canada. Polisi wa Canada walianza kuchunguza dhehebu hilo   miaka ya 1990.