RAIS WA NIGERIA KURUDI BAADA YA WIKI MBILI

0
474

LAGOS, Nigeria


RAIS wa Nigeria, Muhammadu Buhari anatarajia kurudi Nigeria katika kipindi cha wiki mbili zijazo akitokea   Uingereza ambako anapata matibabu.

Taarifa iliyotolewa na Gavana wa jimbo la Imo – Nigeria, Rocha Okorocha ambaye alikuwa miongoni mwa wa ujumbe walioenda kukutana na Rais Buhari Jumapili iliyopita jijini London, alisema Rais huyo anatarajiwa kurudi baada ya wiki mbili

Rais Buhari amekuwa akipata matibabu  Uingereza kwa ugonjwa usiojulikana kwa takribani miezi kadha sasa.

Juzi, Serikali ya nchi hiyo ilitoa picha za Rais Buhari akikutana na magavana kutoka chama chake nchini Uingereza.

 

Picha hiyo ilikuwa mara kwanza kuonyeshwa hadharani akiwa   London tangu aondoke Nigeria zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Okorocha aliambia BBC kuwa, ”Nilikutana na mtu mwenye motisha na anendelea vyema. Hajapoteza ucheshi wake kama anavyojulikana. Kwa hivyo anaendelea vyema na tunafurahi sana kumuona na tunadhani amefanya kitu muhimu kuwahakikishia raia wa Nigeria kuhusu afya ya rais wao”.

 

Wananchi wa Nigeria wamekuwa na wasiwasi kutokana kutokuwa na taarifa sahihi na watu wakidai kwamba huenda amefariki dunia au asirudi tena.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here