24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

V MONEY: NITAJITANGAZA ZAIDI KIMATAIFA

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kizazi kipya,  Vanessa Mdee ‘V Money’, amedai kuwa ataendelea kujitangaza kimataifa ili kuzipa hadhi kazi zake.

V Money ambaye kwa sasa amezidi  kufanya vizuri na kulitangaza taifa la Tanzania, alilipasha MTANZANIA kuwa ili msanii afanikiwe na kupiga hatua lazima ajitangaze.

Alisema kwa kuwa tayari amejikusanyia mashabiki na wapenzi wa muziki wake hapa nyumbani, si vibaya akihamishia nguvu zake nje ya nchi.

“Nitaendelea kujitangaza kimataifa, ndio maana mara nyingi nimekuwa nikisafiri na kufanya mahojiano katika stesheni mbalimbali za redio katika mataifa tofauti tofauti,” alisema V Money.

V money ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘Mapenzi ya Kisela’ aliomshirikisha mwimbaji wa kundi la P Square, Peter Okoye kutoka Nigeria, alisema mipango yake ni kuzidi kufanya kazi na wasanii wakubwa kutoka mataifa tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles