Na MAREGESI PAUL-DODOMA
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiga, ameeleza sababu za Tanzania kuendeleza ushirikiano na taifa la Israel, huku Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akikosoa hatua hiyo akitaka nchi iendelee kuunga mkono mataifa yanayoonewa.
Awali balozi Mahiga akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2018/19 ya Sh bilioni 177.006, alisema sera ya Tanzania katika nchi za nje, itaendelea kuwa ya kutochaguliwa marafiki wala maadui na nchi yoyote duniani.
Alisema maeneo yote yenye migogoro, yatatatuliwa kwa vikao na siyo kwa njia ya vita.
Misingi ya Tanzania kimataifa ni kuheshimika, kulinda utu na kulinda uhuru wa watu. Kwa hiyo, ikitokea mahali fulani watu wananyanyaswa, lazima hao wapewe haki kwanza.
Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.