24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

OFISA ITIFAKI KORTINI KWA KUMSHAMBULIA MWANDISHI

Na JANETH MUSHI-ARUSHA


OFISA Itifaki katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Swalehe Mwidadi (32) na mfanyakazi wa Masijala katika ofisi hiyo, Amina Mshana (29), wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka mawili ikiwamo kosa la udhalilishaji kwa kumvua nguo na kumpiga picha mwanahabari Lucas Myovela, akiwa uchi.

Washtakiwa hao walifikishwa kortini jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda, ambapo Wakili wa Serikali Sabina Silayo, alidai kuwa katika shitaka la kwanza watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha kinyume na sheria.

Alidai kuwa Mei 13, mwaka huu katika eneo la Sakina jijini Arusha, washtakiwa hao waliiba simu mbili aina ya Tecno C 7 yenye thamani ya Sh 300,000 na Samsung yenye thamani ya Sh 50,000, fedha taslimu Sh 75,000, fedha kupitia M-pesa Sh 9,500 na kadi ya benki ya CRDB mali za Myovela

“Kabla na baada ya wizi huo mlitumia panga na mkanda wa plastili kumtishia,” aliongeza Wakili huyo

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles