29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

ZAIDI YA WANAWAKE 1,000 NCHINI HUPATA FISTULA KWA MWAKA

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Wanawake wapatao 1,200 hadi 1,500 nchini, wanakadiriwa kupata ugonjwa wa fistula kila mwaka.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA-Tanzania), Jacqueline Mahon amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa Hospitali ya CCBRT na Shirika lisilo la Kiserikali la Amref.

Mahon amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Fistula Duniani ambayo hufanyika Mei 23, kila mwaka ambapo amesema takwimu zinaonesha pia kila siku zaidi ya wanawake 800 duniani hupoteza maisha kutokana na matatizo yatokanayo na ujauzito.

“Kati yao, wanawake 20 au zaidi hupata majeraha au ulemavu mojawapo ya majeraha hayo ni tatizo la fistula ya uzazi na inakadiriwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni mbili wanaishi na tatizo hilo duniani hasa katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia na Uarabuni,” amemesema.

Mkurugenzi wa CCBRT, Brenda Msangi amesema bado kuna changamoto ya idadi ya  madaktari wa kutibu tatizo hilo ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa waliopo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema suala la mimba za utotoni ni kikwazo katika kutokomeza tatizo hilo.

“Takwimu zinaonesha asilimia 60 pekee ya wajawazito ndiyo huhudhuria lliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu,” amesema Dk. Ndugulile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles