22.4 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ubunifu Lugalo Gofu wamkosha Jenerali Mkunda

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Jacob Mkunda amefurahishwa na ubunifu unaondelea kufanywa na Klabu ya Gofu Lugalo ambao umewavutia wachezaji wengi kushiriki katika shindano la NMB CDF Trophy 2023.

Akizungumza wakati wa kufunga shindano hilo Septemba 3,2023 kwenye viwanja vya gofu Lugalo, Dar es Salaam, Jenerali Mkunda amewapongeza waandaaji, wachezaji huku akiwashukuru wadhamini wote waliojitokeza.

‘Naishukuru Klabu ya Gofu Lugalo na ninawapongeza waandaaji wa mashindano haya chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo kwa kutumia ubunifu wa kuwaleta karibu wapenzi wa mchezo wa gofu hapa nchini na jirani zetu wa Malawi.

“Tumeambiwa kwamba safari hii mwamko ni mkubwa sana, wachezaji zaidi wamejitokeza, tunataka muendelee na mwamko huu.

“Timu yetu ya Lugalo mwaka huu itashirki mashindano ya gofu ya majeshi huko nchini Marekani, ni imani yangu kuwa Lugalo itawakilisha vyema na mafanikio yake ni mafanikio ya Taifa kwa ujumla,” ameeleza Jenerali Mkunda.

Naye Mwenyekiti wa klabu hiyo, amesema licha ya idadi wa wachezaji kuwa kubwa lakini wamemudu kuwahudumia, huku akiahidi kukaa wataalamu mashindano ili mwakani washirikishe watu wengi zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB ambao ndiyo wadhamini wakuu, Filbert Mponzi amesema pamoja na kudhamini kwa miaka nane mfululizo, wataendelea kwa miaka mingine.

“Zamani tulikuwa tunasema CDF Trophy lakini Sasa mashindano haya yanaitwa NMB CDF Trophy, ina maana NMB tutaendelea kuwa wadhamini wakuu,” amesema Mponzi.

Mshindi wa jumla kwa wanaume ni Michael Masawe na wanawake ni Vicky Elias, wote kutoka klabu ya Lugalo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles