24.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani Nyansika ahamasisha wananchi ujenzi kituo cha polisi

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Wananchi wa Kata ya Kivule wamekubaliana kuchangishana Sh 2,000 kila mmoja kumalizia ujenzi wa kituo cha polisi ambao umesimama kwa miaka 15.

Hatua hiyo inafuatia baada ya Diwani wa Kata ya Kivule, Nyansika Getama, kuja na kampeni ya ‘Jenga kituo cha polisi kwa tofali mbili’.

Wananchi wa Kata ya Kivule wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya kata hiyo.

Makubaliano hayo yamefikiwa Septemba 3, 2023 wakati wa mkutano wa hadhara uliohitishwa na diwani huyo na kufanyika katika viwanja vya ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo.

Katika mkutano huo wananchi waliunda kamati ya watu watano itakayohusika kuusanya michango hiyo ambapo wengine walianza kuchangia papo hapo huku Diwani Nyansika akichangia Sh 500,000.

“Tunataka kituo cha polisi kwa sababu tuna shule za sekondari tano, shule za msingi sita, hospitali ya wilaya, watu wakiiba kwenye hizo taasisi tutakimbilia polisi. Tuanze tu kujenga wenyewe tukisema hadi tuwe na bajeti hatutafika,” amesema Nyansika.

Baadhi ya wakazi wa kata hiyo, Gabriel Chacha, Adventina Ishengoma wamempongeza diwani huyo kwa kuja na kampeni hiyo na kuwoamba wakazi wengine kumuunga mkono ili kufanikisha ujenzi wa kituo hicho.

“Tunahitaji kituo cha polisi kwa sababu mji wetu umekua kwahiyo usalama wetu na mali zetu ni wa muhimu, wazo hili ni zuri tumuunge mkono diwani wetu ili tukamilishe ujenzi wa kituo,” amesema Ishengoma.

Katika hatua nyingine diwani huyo amewataka wafanyabiashara katika eneo la Fremu Kumi kuendelea na shughuli zao hadi Soko la Kivule litakapokuwa na miundombinu mizuri.

Ametoa agizo hilo baada ya Kiongozi wa Wafanyabiashara Fremu Kumi, Michael Uronu, kudai kuwa wametakiwa kuhama eneo hilo kwenda Kivule sokoni.

“Soko lina mambo mengi yanayohitajika, tumetengeneza kamati halafu tunataka kutimua watu…tuwe na subira, tuwe viongozi wa kuona hitaji la watu, tuwe na ubinadamu,” amesema Nyansika.

Katika mkutano huo pia wananchi wamelalamikia gharama za kuunganishiwa maji kuwa kubwa hadi kufikia Sh 200,000 ambapo diwani amekiri kufahamu changamoto hiyo na kuahidi kufuatilia katika mamlaka husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles