24.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania na India sasa ni washirika wa kimkakati

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kulingana na Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania mapema leo Oktoba 9, India na Tanzania sasa zimebadili uhusiano wao kutoka wa kawaida Kidiplomasia kuwa wa mkakati.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inayoendelea nchini India ambapo leo imetangazwa rasmi kwenye mkutano wake na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.

Tofauti kati ya ushirikiano wa kidiplomasia na ule wa kimkakati – hasa unaohusu India, ni kwamba nchi zote zinakuwa zimechagua maeneo mahususi ya kushirikiana yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Mazungumzo ya kufikia kufanya biashara kwa kutumia Shilingi na Rupia na kuongeza ushirikiano kwenye huduma za afya, ulinzi na kubadilishana taarifa sasa yatawezekana kwa sababu ya Tanzania na India kufikia hatua hii.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Diplomasia ya Tanzania chini ya Rais Samia ikizingatiwa kuwa haya ni makubaliano dhidi ya nchi tajiri na yenye ushawishi mkubwa duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles