29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA DAIMA KIFUNGONI SIKU 90

Serikali imelifungia gazeti la Tanzania Daima kwa muda wa siku 90 kuanzia leo kwa kuandika habari ya uongo katika toleo lake la 4706 la Oktoba 22, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi, habari hiyo imeupotosha umma kwa kiasi kikubwa na kuleta taharuki huku ikikiuka kifungu cha 54 (1) cha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016.

Taarifa hiyo imesema Mhariri wa Tanzania Daima aliomba radhi kwa upotoshaji uliofanywa katika habari hiyo huku akikiri kosa.

“Hata hivyo, pamoja na kuomba radhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametumia mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari baada ya jitihada za muda mrefu za serikali kuwashauri na kuwakumbusha wahariri wa gazeti hilo kuhusu wajibu wa kufuata misingi ya taaluma na sheria,” amesema.

Pia, taarifa hiyo imeorodhesha baadhi ya habari zilizochapishwa katika gazeti hilo: ‘Dangote aivuruga serikali’ ‘Polisi wasaka Bomberdier kwa Lissu’ ‘Makinikia pasua kichwa’.

“Pamoja na gazeti lako kuomba radhi mara kwa mara na kurejea kwenye uandishi ule ule wenye utata, naona sasa uamuzi wa leo wa serikali utasaidia kuifanya ofisi yako itafakari vizuri kuhusu mwelekeo wake na kujirekebisha kwa kuzingatia misingi ya taaluma ya habari na sheria za nchi,” imesema taarifa hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles