Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â
JUMLA ya wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisaha viungo na makovu katika kambi maaalum ya upasuaji iliyofanyika kwa siku tatu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila.
Upasuaji huo ambao umefanywa na wataalamu wa Hospitali ya Mloganzila kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka Korea Kusini Prof Jeong Tae Kim ulihusisha wagonjwa ambo wameathirika na majanga ya moto, ajali za barabarni pamoja na watoto waliozaliwa wakiwa na hitilafu kwenye viungo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru alimshukuru Prof Kim kwa kujitoa kwake kuja nchini kushirikiana na wataalamu wa ndani kwa lengo la kutoa huduma na pia kubadilishana ujuzi ili kuendelea kutoa huduma bora za kibingwa .
Prof. Museru alisema lengo la hospitali ni kuendelea kuboresha huduma za kibingwa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa wa kutibiwa nje ya nchi.
Awali Daktari Mbobezi wa Upasuaji wa kurekebisha viungo katika Hospitali ya Mloganzila Dk. Laurian Rwanyuma alisema hii ni mara ya kwanza upasuajia huo kufanyika hospitalini hapo tangu ilipozinduliwa rasmi na serikali.