31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ripoti yabaini kikwazo elimu kwa mtoto wa kike

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

RIPOTI ya utafiti kuhusu elimu msingi kwa wasichana ikiangazia sababu zinazokwamisha kuendelea kuwa shule imezinduliwa huku ikionesha maeneo matatu ambayo yanamkwamisha mtoto wa kike kumaliza elimu msingi  ikiwemo mazingira ya nyumbani kutokuwa rafiki.

Ripoti hiyo ilizinduliwa jana jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Leonard Akwilapo.

Utafiti huo umefanyika katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Lindi na Tabora.

Akisoma ripoti hiyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),  Dk. Mugisha Lucius alisema ripoti hiyo inaonesha kwamba sababu zinazowafanya watoto wa kike kushindwa kumaliza elimu  ya msingi ni pamoja na mazingira ya nyumbani kutokuwa rafiki.

“Mwanafunzi anapolelewa unakuta hana nafasi ya kusoma, kazi nyingi za nyumbani, hivyo anaona bora aache shule na kuendelea na mambo mengine hii ni sababu kubwa inayochangia mtoto wa kike ashindwe kuendelea na masomo,” alisema

Mhadhiri huyo alizitaja sababu zingine kuwa ni mazingira ya shule anayosomea kutokuwa rafiki ikiwemo miundombinu pamoja na upatikanaji wa chakula pamoja na kutokujitambua.

“Kutembea umbali mrefu,kukosa chakula shuleni,kuanza mahusiano,jinsi ya kujikinga na hedhi hizi pia ni sababu zinazofanya watoto wa kike washindwe kumaliza elimu ya msingi,” alisema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Haki Elimu, Dk. John Kalage, alisema wameamua kufanya utafiti huo kutokana na idadi kubwa ya watoto wa kike kushindwa kumaliza elimu ya msingi hivyo kuamua kutafuta tatizo kwa kina ni nini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Akwilapo,  alisema bado kuna changamoto ya idadi ya wanafunzi wa kike wanaomaliza elimu ya msingi kuwa chini ukilinganisha na wanaume.

“Wanafunzi wa kike baadhi wanaishia njiani hivyo wito wangu kwa jamii wapewe nafasi ya kusoma majumbani, tusiwabague tuwape fursa,” alisema.

Alisema kumekuwa na jitihada za dhati kuhakikisha watoto wa kike wanamaliza elimu ya msingi kwa kuweka adhabu kali wale wanaowasababishia ikiwemo kuwapa mimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles