24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Sita wafanyiwa upasuaji wa kurekebisha viungo Mlonganzila

Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM                                                     

JUMLA ya wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisaha viungo na makovu katika kambi maaalum ya upasuaji iliyofanyika kwa siku tatu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila.

Upasuaji huo ambao umefanywa na wataalamu wa Hospitali ya Mloganzila kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka Korea Kusini Prof Jeong Tae Kim ulihusisha  wagonjwa ambo wameathirika na majanga ya moto, ajali za barabarni pamoja na watoto waliozaliwa wakiwa na hitilafu kwenye viungo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru alimshukuru Prof Kim kwa kujitoa kwake kuja nchini kushirikiana na wataalamu  wa ndani kwa lengo la kutoa huduma na pia kubadilishana ujuzi  ili kuendelea kutoa huduma bora za kibingwa .

Prof. Museru alisema lengo la hospitali ni kuendelea kuboresha huduma  za kibingwa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa wa kutibiwa  nje ya nchi.

Awali Daktari Mbobezi wa Upasuaji wa kurekebisha viungo katika Hospitali ya Mloganzila  Dk. Laurian Rwanyuma alisema hii ni mara ya kwanza upasuajia huo kufanyika hospitalini hapo  tangu ilipozinduliwa rasmi na serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles