23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 11, 2024

Contact us: [email protected]

Shule ya Brookside ya Kimara Suka Mlipaji kinara wa kodi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shule ya Msingi Brookside iliyopo Kimara Suka, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam imedhamiria kuendelea kuwa mlipaji mzuri kwa kodi kwa lengo la kuchangia maendeleo ya taifa letu.

Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shule ya Awali na Msingi ya Brookside, Masanja Maduhu akiwa amesimama na tuzo ya mlipaji kodi bora kwa mwaka huu, tuzo hizo zilikabidhiwa hivi karibuni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam kwa walipaji kodi bora hapa nchini.

Hivi karibuni shule hiyo ilikabidhiwa tuzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam ikiwa ni miongoni mwa mwa walipaji kodi bora hapa nchini.

“Shule yetu imedhamiria kuendesha biashara zake kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa taifa, anasema Meneja wa Shule hiyo, Masanja Maduhu.

Meneja huyo anasema kuwa shule yake imedhamiria kuendelea kutoa elimu bora kwa wakazi wa Kimara, Wilaya ya Ubungo na maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

“Natoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kuleta watoto wao kwenye shule yetu kwani tunawahakikishia elimu bora kwa  vijana wao,” amesema.

Shule hiyo inatoa elimu ya Awali na Msingi na kwamba wamedhamiria kuendelea kutoa elimu bora kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles