29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Yonazi aridhishwa na maandalizi ya Kuelekea Siku ya UKIMWI Duniani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea maandalizi yaliofanywa na wadau mbalimbali kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika Desemba 1,2023 katika Viwanja vya Morogoro Sekondari ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI”

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo na kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles