Juliana Samwely, TUDARCo
Msanii kutoka lebo ya wasafi, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amesema ikitokea nafasi ya kuchora tattoo atachora ya mpenzi wake Paula Kajala.
Rayvanny atoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Big Sunday Live jana baada ya kuonekana amechora tattoo ya lebo yake mpya.
Sababu ya kumtaja Paula ni baada ya kuulizwa maswali hukuhu mzazi mwenzake Fayvanny na mpenzi wake wa sasa kuwa nani anampa nafasi kubwa.
Hata hivyo amesema hawezi kuchagua kuwa nani anamkubali zaidi kutokana na heshima anayowapa wote.