25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Nandy, Zuchu wachuana AFRIMMA

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

WASANII  wanaotamba katika Bongo Fleva nchini, Faustina Charles ‘Nandy’ na Zuhura Othuman ‘Zuchu’, wameingia kwenye mchuano wa kuwania  tuzo za AFRIMMA kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki .

Kutokana na mchuano huo, wasanii hao wameanza kuwagawa mashabiki katika mitandao ya kijamii kila mmoja akiwa na timu yake inayohamasisha kumpigia kura.

Hali hiyo  inatokana na wanadada hao kuachia nyimbo kali hivi karibuni, zinazoonekana kupendwa na kuwa na mashabiki wengi.

Nandy anatamba na kibao chake cha ‘Acha Lizame’ alichomshirikisha Harmonize, wakati  Zuchu akitamba na wimbo wa Nisamehe.

Tofauti na Zunchu na Nandy, katika kipengele hicho pia wapo wasanii wengine  wa Afrika Mashariki  kama vile  Nadia Mukami (Kenya), Tanasha Donna (Kenya), Maua Sama (Tanzania), Rosa Ree (Tanzania), Vimka (Uganda) na wengine wengi.

Tuzo hizo zilizokuwa na vipengele mbalimbali, zinatarajiwa kutolewa Novemba 15, mwaka huu nchini Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles