30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ni wakati Tanzania kujitangaza 


Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

SOKA ni mchezo unaoendelea kupendwa na kukubalika zaidi duniani kote, hata watoto wadogo wamekuwa wakionyesha mapenzi yao ya dhati juu ya mchezo huo.

Tanzania mwaka huu unaweza kuwa mzuri kwetu kama wachezaji wataendelea kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika klabu zao hadi timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

Simba na Taifa Stars zimeweza kuonyesha jinsi gani hivi sasa soka la Tanzania linaweza kupiga hatua na kulitangaza taifa duniani.

Hongera kwa wachezaji wanaounda vikosi vya timu hizo, lakini ushindani unaoonyeshwa sasa unapaswa kuonekana katika klabu zote zinazoshiriki ligi mbalimbali hapa nchini.

Nidhamu ya wachezaji ni kitu muhimu sana kinachotakiwa kusimamiwa na kupewa kipaumbele zaidi kwa sasa ili kuhakikisha Tanzania tunasonga mbele.

Viongozi wa soka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), viongozi wa klabu, wadau wa mchezo huu kwa pamoja tunapaswa kuonyesha ushirikiano na usimamizi wa karibu kuendeleza lulu tuliyoipata.

Itapendeza kusikia Simba wanafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Stars pia ikionyesha kiwango safi na kutwaa taji katika Michuano ya Afrika (Afcon).

Mbali na timu hizo mbili, pia mwaka huu tunakabiliwa na Fainali za Michuano ya Afrika ya Vijana (Afcon) ambayo itafanyika hapa nchini.

Ushirikiano ulioweza kuonyeshwa kwa Simba na Taifa Stars, unatakiwa kuonekana kwa kikosi cha vijana cha Serengeti Boys ambayo itashiriki fainali hizo.

Tumekuwa ni watu wa kushindwa kwa kipindi kirefu, huku timu zetu zinazoshiriki michuano mikubwa zikijikuta zinabatizwa majina ya ovyo.

Lakini sasa kila mmoja amerudisha tumaini lake juu ya mchezo huo, hivyo ni vema furaha hiyo ya ushindi ikaendelezwa kwa kila kikosi kinacholiwakilisha taifa ndani na nje ya nchini.

Mwaka huu ni wetu, hivyo wachezaji, viongozi wajipange kuhakikisha tunaendelea kupiga hatua na kuondoa mawazo finyu yaliyojengeka vichwani mwa Watanzania wengi kuwa nchi yetu ni ‘kichwa cha mwenzawazimu’ katika sekta nzima ya michezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles