32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

MSIGWA AMTUNISHIA MSULI NAIBU SPIKA

Na GABRIL MUSHI-DODOMA


MBUNGE wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kusababisha mvutano kati yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Hatua hiyo ilikuwa baada ya Dk. Tulia kumwagiza Msigwa kufuta mchango wake wote au baadhi ya maneno aliyozungumza kuhusu mfumo wa utendaji wa Rais John Magufuli.

Msigwa alisema haingii akilini kuona matatizo ya maji vijijini ili yatatuliwe ni  mpaka Rais apige simu kwa katibu mkuu wa wizara na kumuunganisha na mtendaji wa kijiji kutatua tatizo hilo.

“Tunaona ni jambo la kawaida kabisa! Na huyu katibu wa wizara ambaye juzi nilisema badala ya kusimamia utendaji wake amekazana kugombana kwenye mitandao na maaskofu this is a serious business haijawahi kutokea kwa katibu mkuu wa wizara,” alisema na kuongeza:

“Hivi inaingiaje akili kwamba katibu wa wizara unamuunganisha na mtendaji wa kijiji, inaonyesha kwamba mfumo wa serikali umefeli haufanyi kazi, tunafanya majukumu mazito ila hili la maji ni zito zaidi”.

Msigwa alisema tatizo la maji nchini ni kikwazo kikubwa cha kuja watalii nchini kwa kuwa wanaona wananchi wanaovyougua magonjwa ya uchafu kikiwamo kipindupindu kwa sababu ya kukosa maji.

Alisema anaungana na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika  (Chadema), kuhusu pendekezo la kuundwa   kamati maalumu ya uchunguzi wa miradi ya maji nchini.

Lakini wakati Msigwa akiendelea kuchangia, alikatishwa na Dk. Tulia baada ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jensiter Mhagama kutoa taarifa kuwa mchango wa Msigwa ulikuwa unavunja kanuni za Bunge na Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mhagama: “Ni shida   kuendelea kumuona Msigwa akiendelea kuzungumza vitu ambavyo vinavunja utaratibu kwa mujibu wa kanuni kama anavyoendelea kufanya…niendelee kukumbusha kanuni ya 64 (1) kwamba madaraka aliyopewa Rais ni madaraka ya  katiba na anaweza kusimamia jambo lolote wakati wowote kwa utaratibu wowote anaoona unafaa kwa muktadha wa maendeleo ya watanzania.

“Lakini kanuni zetu ndani ya bunge zinaendelea kutukumbusha  kuwa mbunge unapozungumzia jambo lolote hapa ndani, usizungumzie mwenendo wa rais ambaye amepewa kwa mujibu wa katiba ambayo tunayo hapa ndani.

“Kuacha jambo hili liendelee kwa style ya Msigwa ni kuvunja kanuni za Bunge lakini ni kuingilia madaraka ya rais kwa mujibu wa Katiba.

“Ninaomba mbunge aheshimu kanuni ya 64 (1) e kama itakupendeza hayo anayotumia kuzungumzia mwenendo wa rais yafutwe na anapoendelea na mchango wake aheshimu kanuni hizo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles