22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mo akabidhi bilioni 20, apiga dongo

Na Winfrida Mtoi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji(MO) leo Julai 30.202,  amekabidhi  sh 20 billioni  za uwekezaji  katika asilimia 49 ya hisa anazopewa naklabu hiyo katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu baada ya mchakato kukamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, jijini Dar es Salaam, MO amesema katika kipindi cha miaka minne alichokuwa na Simba, ametoa fedha zaidi ya hizo lakini kuna watu wanamsema kuwa hana fedha.

“Mimi kwenye miaka minne nimewekeza sh  bilioni 21.3 na kila pesa ambayo nimetoa ni kwa kutaka mafanikio na kila mwaka nimetoa si chini ya bilioni 5.3, hizi ni pesa za ziada kwa sababu napenda Simba, lakini  kitu kinachoniumiza ni watu kusema MO hana bilioni 20,” amesema.

Ameeleza kuwa mabadiliko yamekamili na kuna vipengere lazima vikamilishwe ambayo ni kutoa fedha zinazotakiwa na amezitoa rasmi.

“Mjue sasa  kwamba sinunui hisa  asilimia 49 kwa bilioni 19.6,  inaweza kufika bilioni 43 au 44 ambayo imezidi kutokana na thamani ya klabu kupanda na imezidi kutokana na uwekezaji.

“Simba ndiyo imeweka mpira wa Tanzania katika ramani ya Afrika, tumetoa timu nne na wenzetu wananufaika na sisi tumefikia malengo yetu,” ameeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles