24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

TFF yawaadhibu Morrison, Mukoko

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewaadhibu wachezaji Bernard Morrison wa Simba na Mukoko Tonombe  wa Yanga kwa makosa waliyofanya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Azam Sports Federation Cup(ASFC) ulikutanisha timu zao Julai 25, 2021 kwenye Uwanja wa  Lake Tanganyika, Kigoma.

Kwa Mujibu taarifa ya TFF, Morrison amepigwa faini ya sh 3,000,000 na kufungiwa mechi tatu kutokana na kosa la kimaadili, nidhamu na udhalilishaji kinyume na kanuni.

Mukoko ametozwa faini  ya  sh 500,000 na kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la la kumpiga John Bocco.

Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Mohammed Nabil, amepigwa faini y ash 500,000 kwa kugoma kuhudhuria mkutano wa maandalizi ya mcheza na  waandishi wa Habari.

Katika hatua nyingine Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh 4 milioni kwa  makosa matatu tofauti, huku viongozi wakipewa onyo kutokana na kukaidi maelekezo na kuingilia utaratibu uliowekwa katika shughuli ya kugawa medali kwa washindi.

Kwa upande wa klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh 4.5 kwa makosa matano tofauti  ikiwamo  viongozi wake  kuingia uwanjani  wakitumia mlango usio rasmi na kuambatana  na watu wasiokuwa na tiketi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles