BILIONEA aliyewahi kuwania kiti cha urais nchini Tunisia, Nabil Karoui, anashikiliwa na polisi wa Algeria kwa kosa la kuingia nchini humo kinyume cha utaratibu.
Karoui (58), ambaye anamiliki kituo cha televisheni cha Nesma TV, aligombea urais katika Uchaguzi wa mwaka juzi, kabla ya kubwagwa na Kais Saied aliyeko madarakani.
Juu ya kukamatwa kwake, alidakwa akiwa na watu wengine wanne mjini Tebessa, eneo lililoko mpakani mwa Tunisia na Algeria.
Majanga hayo yanakuja huku mwanasiasa huyo akitarajiwa kupanda kizimbani kujibu mashitaka ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi.