Na Brighiter Masaki
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amevielekeza vyombo vya dola kumkamata mkurugenzi wa kampuni ya upimaji wa ardhi ya Geolink Solution Tanzania LTD kwa tuhuma za kukusanya fedha za wananchi zaidi ya sh. 18 milioni na kuingia mitini.
Fedha hizo za wananchi wa eneo la mtaa wa Mbezi kati zilikuwa kwa ajili ya upimaji wa ardhi.
Akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kusikiliza kero na migogoro ya jimbo la Kawe, Makalla ametoa ameelekezo na kuzitaka kampuni zote zilizochukuwa fedha za wananchi na kuingia mitini wahusika wakamatwe.
“Kampuni zote zilizochukua fedha za wananchi na kuingia mitini wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.” amesema Makalla
Kero ya Wananchi hao zaidi ya 100 wa eneo la Maendeleo mtaa wa Mbezi Kati limeibuliwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo aliejumikana kwa majina ya Frank Mwanga.