26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

RC Kunenge atoa ahadi tamu Pwani

Na Brighiter Masaki

Mkuu wa Mkoa wa Pwani(RC), Abubakari Kunenge, ameahidi kumaliza migogoro ya ardhi katika  mkoa huo.

Kunenge amesema hayo leo  Agosti 30, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kwa  lengo la kufahamiana na kujiwekea malengo ya mpango kazi Ili kuweza kutangaza Mkoa wa Pwani ndani na nje ya nchi  na rasilimali zake.

Aidha amesema mkoa huo una changamoto  ikiwamo upatikanaji wa  habari huku akiahidi  kufungua milango na kushirikiana na vyombo mbalimbali mkoani hapa.

“Hivi karibuni nitafanya  ziara  ndani ya Mkoa wa Pwani,  mimi ni mtawala hivyo nahitaji kutatua changamoto  mbalimbali zinazowakabili wananchi wengi ‘ amesema Kunenge.

Naye Katibu  Tawala wa mkoani humo, Mhandisi  Mwanasha Tumbo amesema kuwa wamewatuma wataalamu mbalimbali katika Wilaya za Bagamoyo na Chalinze ambapo watajihusisha kwa  kung’amua changamoto zinazowakabili wananchi na  kuzitatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles