30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Faraja Deogratias aachia ‘Wewe ni Mwema’

ARIZONA, MAREKANI

KUTOKA Phoenix, Arizona Marekani, mwimbaji wa Injili, Faraja Deogratias, amewaomba wapenzi wa muziki huo kuendelea kusikiliza na kutazama video ya wimbo mpya, Wewe ni Mwema.

Akizungumza na MTANZANIA, Faraja alisema anashukuru mapokezi ya awali ambayo ameyapata alipoachia video hiyo inayochezwa kwenye runinga mbalimbali Afrika Mashariki.

“Meseji ya wimbo huu inazungumzia wema wa Mungu maishani mwangu kwa sababu wema wake umeniheshimisha na kuniinua, naamini utawabariki wengi ambao Mungu amewafanya wawe na heshima na kuwainua kwenye jamii yetu, nimemshirikisha mwimbaji mwenzangu Alphonce Mutema,” alisema Faraja mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles