TOKYO, JAPAN
VIONGOZI wa China, Japan na Korea Kusini wamekubaliana kushirikiana kutafuta amani katika Rasi ya Korea na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia za kuitaka Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia.
Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, walikubaliana kushirikiana wakati ambao Korea Kusini na Korea Kaskazini zinaelekea katika mchakato wa kupatikana kwa amani ya kudumu eneo hilo.
Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa pande tatu unaofanyika mjini Tokyo, Japan, ambapo mkutano wa mwisho wa aina hiyo ulifanyika mwaka 2015 mjini Seoul, Korea Kusini.
Suala la Korea Kaskazini lilitawala Katika mkutano huo, baada ya mkutano wa kihistoria kati ya Moon na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un mwezi uliopita.
Viongozi wa mataifa hayo matatu yenye nguvu barani Asia, ambao uhusiano wao wakati mwingine uligubikwa na mzozo wa kikanda na kihistoria pia walijadiliana masuala ya kiuchumi kipindi ambacho Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza shinikizo la kibiashara kwa China na Japan.
Pia wamekubaliana Korea Kusini na China zinaweza kuanza kufanya utafiti wa pamoja kuhusu uwezekano wa kuwepo miradi ya reli itakayoziunganisha nchi hizo.
Aidha, Moon na Keqiang wamekubaliana kuwa Korea Kaskazini inapaswa kupewa msaada wa kiuchumi itakapoachana na mpango wake wa silaha za nyuklia.
Pia wamekubaliana kuwa jumuiya ya kimataifa ikiwemo Marekani zinapaswa kuihakikishia Korea Kaskazini mustakabali mzuri, kama vile usalama wa serikali na