29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI KULETA MWEKEZAJI MWINGINE UDART

Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali iko kwenye mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine wa Mradi wa mabasi ya Mwendokasi (UDART) ili kuimarisha usafiri jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo ameitoa bungeni leo Mei 10, jijini Dodoma akijibu swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu lililoulizwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulidi Mtulia (CCM).

Katika swali lake Mtulia amedai Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha mfumo wa usafiri hasa mabasi ya Mwendokasi katika Jiji la Dar es salaam lakini bado usafiri ni changamoto jijini humo ikiwamo mgogoro kati ya mwendeshaji na Maxmalipo na miundombinu kuharibika.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali  inaendelea kuondoa changamoto za mwendeshaji aliyepo sasa lakini wameanza utaratibu wa kupata mwekezaji mwingine ambaye ataingiza mabasi yake.

“Pale Makao Makuu ya UDART kwa sasa ni mapito ya maji kutokana na mvua kuwa nyingi, mgogoro anaousema popote pale kunapokuwa na taasisi mbili zimeunganishwa kuwa chombo kimoja kunakuwa na migogoro ya ndani lakini Serikali tutalisimamia hili.

“Jambo hili linaendelea kufanyiwa kazi na mfumo huu wa UDART unaingia kwenye awamu ya pili uendeshaji na tutatafuta mbia mwingine aingize mabasi yake ili kupata huduma bora kwa maana ya ushindani ili kuwe na huduma bora zaidi.

“Sisi tunaamini mwendeshaji mmoja anapoleta matatizo kama kuna mwekezaji mwingine anajiimarisha ili kuondoa yote ya uendeshaji pale ambapo itabainika mwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri, tunamwondoa,” amesema Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles