29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Bado hamjasema; washindi 40 mtoko wa kibingwa ndani ya Derby ya Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Hatimaye washindi 40 Promosheni ya 8 ya Mtoko wa Kibingwa wamepatikana ambapo sasa wataitazama Derby ya Kariakoo inayozikutanisha Simba na Yanga Jumapili hii Novemba 5, 2023 katika uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Novemba 4,2023 Afisa Habari wa Betika Tanzania, Juvenalius Rugambwa wakati akiwapokea washindi hao kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam amesema washindi hao wamepatikana kupitia droo ya Mtoko Kibingwa iliyoanza mapema Oktoba, mwaka huu.

Mshindi wa Mtoko wa Kibingwa na Betika msimu wa tatu, Juma Makalani akizungumza na Wanahabari leo Novemba 4,2023 baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kushuhudia Derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga Novemba 5,2023 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

“Kama mnavyowaona hawa ni washindi ambao wamepatikana kupitia kampeni yetu ya mtoko wa kibingwa na hawa washindi 40 waliowasili leo wataenda kuungana na wenzao wa Dar es Salaam na kukamilisha idadi kamili ya washindi 40 na wote watakwenda kulala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

“Na kesho wakiamka watakula chakula kizuri baada ya hapo watapelekwa na ving’ora uwanja wa Benjamini Mkapa kuitaza Deby ya Kariakoo inayozikutanisha Simba na Yanga wakiwa wameketi katika jukwaa la watu maalum (VIP),” amesema Jevenalius.

Jevenalius amesema kampuni ya Betika imekuwa ikitoa ushindi hapo hapo pia itaendelea kuonesha nia yao ya dhati ya kunyanyua michezo kuanzia mpira wa miguu hadi kutoa udhamini katika michezo mbalimbali.

“Kama tulivyo sisi mshindi akishinda anapewa zawadi zake hapohapo kwa haraka, tunawaomba watu waendelee kutupia ubashiri kwa kutembelea kwenye tovuti yetu hata hii mechi ya Simba na Yanga ipo hapo,” amesema.

Nao baadhi ya washindi hao akiwemo, Juma Makalani kutoka mkoani Mtwara pamoja na Michael Kawala kutoka Sumbawanga mkoani Rukwa wameishukuru kampuni ya Betika kuwapa fursa ya kuitazama Deby hiyo ya Simba na Yanga, kwani ilikuwa ndoto yao.

“Kweli Betika hawana longolongo kwa mara ya kwanza nimepanda ndege hata nilipoambiwa nimeshinda sikuamini, nawashukuru sana Betika,” amesema Kawala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles