24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali yaua watumishi watano B’moyo

Na Mwandishi Wetu

WATUMISHI watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamepoteza maisha baada ya kupata ajali mbaya ya gari iliyohusisha  magari manne jana.

Shuhuda wa ajali hiyo, ameiambia MTANZANIA kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori la mchanga, lililokuwa likijaribu kuipita gari dogo ghafla ikakutana na msafara wa magari hayo ambayo yalikuwa yameongozana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za Mitaa.

Shuhuda huyo, alisema baada ya gari  ndogo aina ya Vitz yenye namba za usajili T 598 DES kulipita lori hilo lenye namba za usajili T238 CCW lililokuwa likiendeshwa na  Josephat Eliyatinga katika eneo la Darajani Mapinga, ghafla lilikutana na msafara huo na dereva wake kushindwa kufunga breki.

Alisema lori hilo liligongana uso kwa uso na  magari ya  Nissan Patrol yenye namba za usajili SM 10414 na Land Rover 110 yenye namba za usajili STL 1620 mali ya halmashauri.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya miili ya majeruhi na maiti kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Amiri Batenga alithibitisha vifo vya watu wanne na majeruhi 10.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Halid Hassan (40) dereva wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Makame Ally (40) dereva  kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara ya Mipango wa halmashauri hiyo, Tunsiime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya na Ludovick Palangyyo, ambaye ni Mchumi wa Halmashauri.

Aliwataja majeruhi waliopata huduma ya kwanza na baadaye kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo (DED), Ibrahimu Matovu aliyevunjika mguu, Mhandisi wa Maji, Juliana Msaghaa ambaye amejeruhiwa vibaya, Mweka Hazina, George Mashauri ambaye amepata majeraha usoni, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Julius Mwanganda ambaye amevunjika mkono.

Wengine ni Mshauri wa TASAF Bagamoyo, Amadeus Mbuta, Mratibu wa TASAF, Doroth Njetile aliye alivunjika miguu yote, Tauliza Halid na Amari Mohamed wananchi wa kawaida.

Batenga alisema Ofisa Utumishi wa Wilaya hiyo, Grace Mbilinyi  alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

“Tumepokea majeruhi, hali zao ni mbaya tumewahamishia Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi,”alisema Dk. Batenga.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Tamisemi) Selemani Jaffo alisema wamepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa.

“Tumepoteza watalaamu wetu, wajumbe wangu wamepata mshtuko mkubwa, tunamwomba Mungu awapokee,”alisema Waziri Jaffo.

Alisema Serikali itahakikisha inagharamia gharama zote ili majeruhi wa ajali hiyo wapate tiba inayostahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles