29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Dampo la Nsalaga Uyole hatari kwa afya

Na MWANDISHI WETU -MBEYA

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima,  ameghadhibishwa na ujenzi duni wa dampo la taka la Nsalaga Uyole, mkoani Mbeya, na kuonya kwamba miundombinu hni hatari kwa afya za watu na mazingira kwa ujumla.

Kutokana na hali hiyo amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC),  kushirikiana na ofisi za Mkoa wa Mbeya ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo kwani dampo hilo limejengwa bila kuzingatia kanuni za kuhifadhi mazingira.

Pamoja na hali hiyo pia utupaji taka kwenye dampo umekuwa ukirudidha uchafu kwenye makazi ya watu.  taarifa alizopata ni kwamba dampo limejengwa bila utafiti wa kitaalamu wa kutosha.

Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini hapa mara baada ya kutembelea  eneo la Nsalaga Uyole, katika   ziara yake  ya kikazi kukagua uzingatiaji wa  Sheria ya Mazingira, katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Sima alikumbusha kwamba  taka lazima zitenganishwe kwenye vyanzo kabla ya kuingizwa kwenye dampo.

“Kuanzia sasa watafutaji taka wasiruhusiwe kuingia kwenye mashimo ya dampo kwani wamekuwa wakirudisha uchafu kwenye makazi ya watu na kuchafua mazingira,” alisema Sima

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Sima, aliambatana na Mwenyekiti wa  Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC),Profesa Esnati Chaggu, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka pamoja na maofisa  wa NEMC, ambapo aliwataka wasimamizi wa dampo hilo kujifunza kutoka kwa wasimamizi wa madampo katika mikoa mingine ambako  madampo ya kisasa tayari yamejengwa na yanahifadhi  mazingira.

“Halmashauri ya Mkoa wa Mbeya  mjipange na kuhakikisha mnatenga eneo maalum ya shughuli za urejelezaji ili kuondoa  mlundikano wa  uchafu, kwani mmekuwa mkichanganya uchafu na taka ngumu ambazo ni ngumu kuzizoa,” alisema Sima

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NEMC, Prof. Chaggu alisema majitaka yatokayo katika dampo  yana sumu kiasi kikubwa na kufafanua kwamba majitaka hayo yana asilimia nane juu ya majitaka yatokayo majumbani.

Alitaka majitaka hayo yasimamiwe kwa umakini ili yasitiririke katika mazingira na kudhuru jamii inayoishi karibu na dampo hasa katika kipindi cha mvua.

Naye Mkurugenzi wa NEMC, Dk. Samwel Gwamaka alifafanua kwamba kwa mujibu was  Sheria ya Mazingira na Kanuni za Usimamizi wa Taka ngumu, halmashauri za wilaya zina wajibu wa kutenganisha taka na kuelimisha wananchi jinsi ya kufanya hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles