28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Rushwa ya ngono inarudisha nyuma juhudi za mwanamke

Amina Omari,Muheza

RUSHWA ya ngono imeelezwa ni miongoni mwa vitendo vya ukatili ambavyo vinaongoza kurudisha nyuma juhudi za maendeleo ya mwanamke nchini.

Hayo yalisemwa na Ofisa Programu Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripotia habari za jinsia.

Alisema kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) za mwaka 2016/18, zinaonyesha  asilimia 45 ya wanawake kati ya umri wa miaka 15 -49, wamekuwa waathirika wa ukatili wa kijinsia,huku asilimia 25, ikiwa ukatilia wa kuumizwa mwili.

Alisema vitendo vya unyanyasaji wa kingono,vimekuwapo pale ambapo mwanamke anashida ya kutafuta ajira,fursa za kimasomo na hasa nyakati za uchaguzi

“Vitendo hivi vimekuwa vikichangia kuwaumiza wanawake kisaikolojia na ukandamizwaji wao,”alisema Sangai.

Alisema mtandao huo,umekuwa na kazi ya kusaidia kujengea uwezo wanawake ili kutambua haki zake.

Ofisa Habari wa TGNP, Monica John alisema vyombo vya habari vinajukumu la kuhakikisha wasaidia kundi hilo kupata haki zao .

Alisema  kusaidia kundi hilo kutambua haki zao, ikiwamo huduma bora za afya ,ushiriki wa wanawake katika uongozi na chaguzi mbalimbali.

Baadhi wa wanawake wa Kata ya Zirai, walisema mfumo dume wa wanaume kumiliki mali na ardhi, imekuwa ni kikwanzo cha maendeleo ya mwanamke.

“Mwanamke wa vijijini hauna haki ya kushiriki  ngazi ya uamuzi,tukiwa sehemu ya wazalishaji tunabaki tunaangalia tu,”alisema Joice Stanley.

Alisema kuwa licha ya kata hiyo  kuongoza kilimo cha viungo,ubovu wa barabara umekuwa  changamoto ya mazao yao kufika sokoni mapema,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles