30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA DAY KUUNGURUMA KESHO MAPEMA

BETHSHEBA WAMBURA NA ELIZABETH JOACHIM-DAR ES SALAAM

TAMASHA la tisa la klabu ya Simba liitwalo Simba Day, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 6:00 mchana.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Haji Manara, amesema tamasha hilo litaanza mchana kwa mechi kati ya Simba Queen na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Simba.

Manara alisema baada ya mechi hiyo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwamo na bendi ya Twanga Pepeta.

“Kesho tamasha la Simba Day litaanza mapema kabisa, tutaanza saa 6:00 mchana kwa mechi ya timu za Simba ya wanawake na vijana,” amesema Manara.

Baada ya mechi na burudani ndio utafuata utaratibu wa utambulisho wa wachezaji na kisha jioni kutakuwa na mechi yao ya kirafiki dhidi ya timu ya Asante Kotoko kutoka nchini Ghana itakayochezwa jioni.

Kwa upande wao manahodha wa Timu zote mbili, Emos Frimpong (Asante Kotoko) na Aishi Manula (Simba SC), wamesema wamejiandaa vya kutosha na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki.

“Simba ni timu kubwa si tu kwa Tanzania bali Africa kwa ujumla japo mechi hii ni ya kirafiki ila ni mechi ngumu, tunafurahi kuwa hapa ila mashabiki waje kwa wingi kushuhudia mtanange huu,” amesema Frimpong.

Emos Frimpong

Kwa upande wake Manula amesema, “Tulipokuwa Uturuki tulifanya mazoezi ya kutosha tumejiandaa vizuri kwa msimu mpya na mechi ya kesho na mchezo wetu wa kesho utakuwa mzuri tunawaomba mashabiki wa Simba na Tanzania wajitokeze kwa wengi kesho kwa sababu tunacheza na Timu kubwa na ni nafasi yetu kujionesha na kuwazawadia mashabiki wetu,” amesema Manula.

Aishi Manula
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles