29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

RICK ROSS, FAT JOE, T.I WAMKINGIA KIFUA MEEK MILL

NEW YORK, MAREKANI

WASANII mbalimbali wa muziki wa hip hop nchini Marekani, wameungana pamoja na kuonesha sapoti yao kwa mwenzao, Meek Mill, ambaye anaweza kwenda jela miaka miwili hadi minne kwa kukutwa na silaha kinyume na utaratibu pamoja na kujihusishwa na dawa za kulevya.

Wiki iliyopita msanii huyo alifikishwa mahakamani kutokana na kesi hiyo ambayo ilianza mwaka 2009, hivyo kutokana na mashtaka yake kuna uwezekano mkubwa wa kwenda jela.

Rapa Jay Z, Rick Ross, T.I, Fat Joe na wengine wengi wamejitokeza kwa kuonesha sapoti na upendo kwa nyota huyo kutoka Philadelphia.

Jay Z alitumia ukurasa wake wa Instagram na kusema: “Sidhani kama Meek Mill ana kosa lolote, ninaamini tutaendelea kuwa na yeye,” aliandika Jay Z, wakati huo T.I. alisema: “Watu wote wa muziki wa hip hop tupo na wewe, Mungu pia yupo na wewe,” aliandika T.I.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles