26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ado Shaibu: Nitaendelea kuimarisha muundo wa chama

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema wamekusudia kukifanya chama hicho kuwa imara zaidi kuliko vingine na kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa ni kuendeleza kazi ya kuimarisha muundo wa chama.

Ado ameteuliwa kwa mara nyingine kushika wadhifa huo katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kilichokutana Machi 7,2024.

Akizungumza na Waandishi wa habari Machi 8,2024 amesema wanataka kukifanya ACT Wazalendo kuwa chama imara zaidi kuliko vyama vyote vya siasa nchini.

“Ukatibu mkuu wangu hautakuwa wa ofisini, muda wote nitakuwa ‘field’ kuimarisha mtandao wa chama na uongozi nchi nzima.

“Tunataka kukifanya ACT Wazalendo kuwa chama imara zaidi kuliko vyama vyote vya siasa Tanzania. Tunakijenga na kukiimarisha ACT kitaasisi, tunataka tukipimwa katika miaka mitano ijayo kiwe ndio chama bora kuliko vingine katika Bara la Afrika,” amesema Ado.

Kikao hicho pia kiliwateua viongozi mbalimbali ambao ni Omary Shaban (Mwanasheria Mkuu), Bonifansia Mapunda (Naibu Mwanasheria Mkuu) ambaye pia ni Wakili wa Mahakama Kuu na Abdallah Bakari Hassan (Mkaguzi Mkuu wa Ndani).

Wengie ni Rachel Kimambo (Katibu Idara ya Fedha), Salim Abdallah Bimani (Katibu Idara ya Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma) na Shangwe Ayo (Naibu Katibu Habari Uenezi na Mawasiliano ya Umma).

Vilevile wamo Mwanaisha Mndeme (Katibu Mambo ya Nje, Oganaizesheni Mafunzo na Uchaguzi, Shaweji Mketo (Katibu Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi), Pavu Juma Abdallah (Naibu Katibu Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi).

Wajumbe wa Kamati Kuu walioteuliwa ni Mansoor Yusuf Himid, Joran Bashange na Kuluthum Jumanne Mchuchuli. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Taifa, Mary Zacharia na Mgeni Jadi Kadika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles