WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka linalofanyika Machi 28 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Kahama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, amesema Profesa Mbarawa amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo, ambalo linashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.
Msama alisema Profesa Mbarawa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ni ishara kwamba tamasha hilo halijaegemea upande mmoja wa dini kama inavyodhaniwa na baadhi ya wadau wa muziki huo.
“Tunampongeza Profesa Mbarawa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwani huwa halijali dini, jinsia wala kabila katika utekelezaji wake,” alisema Msama.