28.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Profesa Mbarawa mgeni rasmi Tamasha la Pasaka Kahama

4NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka linalofanyika Machi 28 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Kahama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, amesema Profesa Mbarawa amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo, ambalo linashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

Msama alisema Profesa Mbarawa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ni ishara kwamba tamasha hilo halijaegemea upande mmoja wa dini kama inavyodhaniwa na baadhi ya wadau wa muziki huo.

“Tunampongeza Profesa Mbarawa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwani huwa halijali dini, jinsia wala kabila katika utekelezaji wake,” alisema Msama.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,324FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles