BABA wa marehemu Kristina Brown, Bobby Brown, amesitisha maonyesho yake ya kimuziki baada ya kugundulika chanzo cha kifo cha mwanawe, marehemu Kristina.
Bobby alikuwa na ratiba ya kufanya maonyesho katika mji wa Carolina, mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini alisitisha kutokana na kugundulika kwamba mwanawe huyo alifariki Julai mwaka jana kutokana na kuzidisha kilevi cha bangi, pombe na dawa za kuondoa wasiwasi.
“Awali nilikuwa naumwa nikashindwa kufanya shoo kwa kuwa niliamua nipumzike kwa muda, lakini ratiba yangu ilikuwa tayari tangu wiki iliyopita, ila kutokana na taarifa za chanzo cha kifo cha mwanangu nimeshindwa kuendelea na ratiba hiyo,
“Najua mashabiki walikuwa tayari kwa ajili ya shoo, naomba radhi ila baada ya muda nitafanya kile ambacho nilikusudia kukifanya,” alisema Bobby.