Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Bosi wa lebo Cutsleeve Records kutoka Japan, Jdart, ametamba kutikisa ulimwengu wa muziki kupitia kazi yake mpya, Cutsleeve Riddim yenye mkusanyiko wa nyimbo za wasanii kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
Ndani ya Cutsleeve Riddim, Jdart ana nyimbo mbili ambazo ni Believe inayowatia moyo vijana kupambania ndoto zao pamoja na wimbo wa mapenzi unaoitwa Apologies.
Jdart ameiambia www.mtanzania.co.tz kuwa lengo lake ni kubadilisha ulimwengu wa muziki kupitia Cutsleeve Riddim, hivyo anaamini mashabiki wa mataifa mbalimbali watafurahia kazi hiyo mpya.
“Wasanii kutoka Tanzania ni Madematrix, Lody Music, Melodyne na wasanii wa mataifa mengine ni Teejay, Chronic Law, Shatti, Int3ll, Jahvillani, Onsoundmynd, Cashan, Iquu, Zebee, Jah Sam, Slyngaz, B.J Goldman, Iamstylez Music, Galiano, Shakespeare, D-Dondadda na Abijade na muziki umeanzaliwa na maproduza wa Cutsleeve Records na Fraga hapo Tanzania,” amesema Jdart.