25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TBL yamwaga Dola 100,000 kwa kampuni chipukizi za kiuvumbuzi

*Mshindi kuibuka na Dola 100,000

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) inayomilikiwa na kampuni ya AB InBev
imeendelea na jitihada za kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali za
maendeleo kwenye jamii kwa kutoa wito kwa wavumbuzi kujiunga na Programu
yao ya ‘Accelerator 100+’.

Meneja Ugavi wa Kampuni ya TBL, Dickson Rushekya akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza program ya ‘Accelerator 100+’ inayowezesha Kampuni chipukizi za kiuvumbuzi kutoka mikoa yote nchini kujiunga ziweze kupata Dola 100,000 za kimarekani ili kuziwesha kutatua changamoto za kimaendeleo endelevu katika nyanja za ugavi, utunzaji maji, kilimo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Smart Lab, Edwin Bruno na Meneja wa Masuala endelevu wa TBL, Abigail Mutaboyerwa.

Programu hiyo imetangazwa leo Machi 31, 2022 na Meneja wa Masuala endelevu wa TBL, Abigail Mutobiyerwa, ambapo amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wavumbuzi
kutoka mikoa yote nchini kujiunga na program hiyo ili kutafuta suluhisho la
changamoto kwenye ugavi, utunzaji wa vyanzo vya maji na kilimo endelevu na maeneo mengine.

“Programu hii imedhamilia kuwezesha kampuni ndogondogo zenye
shauku ya kufanikiwa kwa kubuni na kuvumbua mawazo yenye tija kwenye jamii
ili kutafuta suluhisho za changamoto za ugavi, utunzaji maji, kilimo, endelevu,
mabadiliko ya tabia nchi, ukuaji wa pamoja na viumbe hai,” amesema
‘Mutobiyerwa.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka ya miwili iliyopita, programu hiyo
imeziongezea uwezo kampuni 70 kwenye nchi zaidi ya 20 na kuwajengea uwezo
wajasiliamali kwa kuwasaidia kupeleka bidhaa zao sokoni kwa haraka.

Amesema TBL imefugua milango kwa kampuni chipukizi kwa ajili ya kujiunga na
programu hiyo itakayowawezesha kupata mafunzo, Ushauri na pesa kiasi cha
dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Chanzi Ltd, Andrew Wallace ambaye aliwahi kuwa
mshindi wa programu hiyo ameshiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao na
kusema kupitia Accelerator 100+ wamekuwa wakikusanya chakula
kinachotupwa na kukibadirisha kuwa chakula cha wanyama na mbolea halisi na
kufanya kazi kubwa ya kuwezesha biashara nyingi kutafuta suluhisho kwa jamii.

Aidha, imeelezwa waombaji wote watafanyiwa tathmini kwa awamu na alama
zimetolewa kulingana na kuendana na changamoto endelevu zilizotambuliwa, uwezo wa kuonyesha kuwa bidhaa inafaa sokoni, ujuzi wa mauzo na timu ya mauzoUwezo wa kufanya majaribio kwenye eneo lolote duniani litakaloteuliwa.

Kwa mujibu wa waandaaji hao, mwisho wa kutuma maombi hayo ni Aprili 30, 2022 kupitia tovuti ya www. 100 Accelerator.com

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles