25.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yaiagiza Serikali kununua mahindi tani 100,000

Na  Ramadhan Hassan, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya awali kukunua tani 24,000  sababu ni kutokana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) kudai kutakuwa na upungufu wa mvua msimu ujao wa kilimo.

Pia, kimeziagiza Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango wakutane kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juzi Septemba 6, jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa (CCM), Daniel Chongolo amesema mwezi wa saba Sekretariet ya CCM ilifanya ziara katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.

Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza serikali kununua mahindi hayo ambapo  ilitoa zaidi ya Sh bilioni 14, ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.

Amedai kwa sasa fedha hizo zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta soko la kuuzia mahindi yao.

Kutokana na hali hiyo Chongolo ameiagiza serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za wakulima hao kwani wanazo taarifa kwamba msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa chache.

“Tena kwa bei ile ile ya Sh 500 kwa kilogramu na wafanye zoezi hilo liwe endelevu kwani mamkala ya hali ya hewa imesema kuna changamoto katika mvua za vuli mpaka katika mvua za masika hivyo kutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula,” amesema.

Pia amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.

“Kuna malalamiko kukatwa  fedha katika Sh 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi, Ileje, Mbozi, Nkasi tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali,” amesema Chongolo.

Katika hatua nyingine, ameziagiza  Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango wakutane kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Amesema kwa sasa bei ya mbolea aina ya Urea imepanda maradufu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona ambapo awali ilikuwa shilingi 50,000 mpaka 55,000 lakini kwa sasa ni Sh 80,000 mpaka 85,000.

“Tunaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango waanze mchakato wa jinsi ya kuwasaidia wakulima.Nasisitiza Wizara zikutane mapema kuwezesha kupungua kwa bei ya mbolea,” amesema.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo amesema mara baada ya maagizo hayo baada ya wiki mbili wataanza ziara ya kukagua maelekezo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles