29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watumia fursa ya Sabasaba kusajili biashara zao Brela

Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAKALA wa Usajili Biashara na Leseni(BRELA) umesema zaidi ya watu 100 wamefanikiwa kusajili biashara na Makampuni katika Maonyesho ya 45 ya biashara ya Kimatafa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es Salaam huku lengo zaidi ni kusajili watu 500.

Baadhi ya Watu wakiwa katika banda la Wakala wa Usajili wa biashara na leseni(BRELA) lilipo katika Maonyesho ya 45 ya biashara ya Kimatafa DITF yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Maonyesho hayo Mkuu wa kitengo cha uhusiano (BRELA) Roida Andusamile amesema toka Maonyesho hayo yalivyoanza hadi kufikia Julai 4 mwamko wa watu kujitokeza katika banda hilo kufanya usajili umekuwa mkubwa sana.

Amesema usajili huo umekuwa ukifanyika kwa njia ya mtandao ambapo BRELA imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa haraka na ufanisi na pindi wanapokamilisha wamekuwa wakipatiwa cheti.

“Mteja akishasajili jina la Biashara au kampuni na kulipia na kutimiza matakwa ya kimsingi anapatiwa cheti ambapo tayari anakuwa amelasimisha biashara yake,”amesema

Amesema mtu anapofanya usajili wa jina la Biashara yake au kampuni anakuwa anauwezo wa kupata fursa mbalimbali ikiwemo kumsaidia pindi anapoitaji kupata mikopo au kuomba dhabuni pindi zinapokuwa zimetagazwa .

Aidha aliwataka watu kuendelea kujitokeza zaidi BRELA ili waweze kupata elimu sambamba na kusajili majina ya kampuni na Biashara zao kwani gharama zake ni ndogo na nafuu sana.

Amesema katika usajili huo wamekuwa wakikumbana na chagamoto ikiwa ni pamoja na watu kutokuwa na tovuti pamoja na kutokutambua vizuri usajili wa Mtandaoni.

Andusamile amesema kutokana na chagamoto hizo BRELA imejipanga kutoa elimu zaidi ambapo tayari imefanikiwa kutoa Mafunzo kwa Maofisa Biashara ili waweze kuwasaidia watu wanapokutana na chagamoto pindi wanaposajili majina ya Biashara na Kampuni .

“Tayari tumefanikiwa kutoa Mafunzo kanda ya kati, Nyanda za kuu ya kisini pia tutaendelea na kanda nyingine ili maofisa Biashara wote wajue jinsi ya kuwasaidia Wafanyabiashara ili waweze kujisajili kwa njia ya mtandao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles