33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Sita wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya watu 17

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Mahakam Kuu Kanda ya Musoma, imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa sita wa mauaji ya watu 17 wa familia moja huku ikiwaachia huru washtakiwa watatu baada ya kukutwa hawana hatua.

Hukumu hiyo ilitolewa Januari 15, mwaka huu na baada ya Jaji Mustapha Siyani kueleza mahakamani hapo kuwa washtakiwa wote sita wamekutwa na hatua ya kufanya mauaji ya wana familia hao kwa kulipiza kisasi cha kuuawa kwa ndugu yao.

Waliohukumiwa kunyongwa ni Juma Mugaya, Aloyce Nyabasi, Nyakaranga Wambura Biraso, Nyakaranga Masemere Mugaya, Sadock Alphonce Ikaka na Kumbasa Buruai Bwire.

Walioachiwa huru ni Marwa Maua Mugaya, Ngoso Mgendi Ngoso na Sura Bukaba Sura.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na mawakili wa serikali watano, Renatus Mkude,Valence Mayenga, Robert Kidando, Ignatus Mwinuka na Yese Temba na upande wa utetezi uliwakilishwa na mawakili tisa.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo namba 56 ya Mwaka 2018 iliyokuwa imepachikwa jina la; kesi ya Mugaranjabo, mlalamikaji akiwa Jamhuri dhidi ya washtakiwa waliokuwa wakikabiliwa na makosa 17 ya mauaji, Jaji Siyami alisema mahakama imewatia hatiani washtakiwa sita.

Jaji Siyami aliiambia mahakama kuwa washtakiwa sita waliotiwa hatiani wanahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na makosa ya kuua kwa kusudia wakiwa wanalipiza kisasi cha kuuawa kwa  Mugaya aliyekuwa akituhumiwa na wananchi kwa wizi wa mifugo.

Ilielezwa Mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Februari 16, 2010 katika eneo la Mugaranjambo lililopo Musoma Mkoa wa Mara.

Washtakiwa walitekeleza vitendo vya mauaji kama sehemu ya kulipiza kisasi cha kuuawa kwa Mugaya mwaka 2005 kwa tuhuma za wizi wa mifugo baada ya mzee wa familia hiyo, marehemu Kawawa Kinguye kupiga yowe wakati wizi wa mifugo unafanyika nyumbani kwake.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa 16 ambapo wengine walifariki vifo vya kawaida wakiwa magereza kabla ya kesi kusikilizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles