26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Sajilini biashara zenu mtambulike- Sorage

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Kaimu Waziri wa biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mudrik Soraga amewataka wafanyabiashara kusajili biashara zao hatua itakayowawezesha kutambuliwa rasmi na kuwa walipa kodi ili kuchangia maendeleo ya Taifa.

Meneja wa benki ya NMB Tawi la Zanzibar, Abdalla Duchi (kushoto) akipokea cheti kutokana na benki hiyo kudhamini maonyesho hayo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Soraga ambae pia ni Kaimu Wizara ya Biashara viwanda na masoko Zanzibar.

Alisema hayo alipokuwa akilifunga Tamasha la Saba la Biashara la Zanzibar kwenye viwanja vya Maisara, Zanzibar Tamasha ambalo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kusherehekea Maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo kwa mwaka huu yametimiza miaka 57.

Soraga ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji amewasihi wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kushiriki matamasha mbalimbali ya biashara ya ndani na nje ili kuwaongezea uzoefu hatua itakayowawezesha kupanua wigo wa soko la bidhaa zao na kujiongezea kipato wao binafsi na Taifa kwa ujumla.

“Tuna adhma ya kuwaalika wafanyabiashara wa Mataifa mengine kushiriki Tamasha hili katika miaka ijayo hatua itakayolifanya kuwa la Kimataifa na kuongeza wigo kwa wafanyabiashara wa ndani kujifunza zaidi,” amesema Soraga.

Aidha, Katika hafla hiyo, Soraga alikabidhi tuzo kwa Benki ya NMB na taasisi kadhaa ambazo zilidhamini Tamasha hilo la Saba la Biashara la Zanzibar.

Akizungumza baada ya kupokea Tuzo, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar, Abdalla Duchi amesema benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa lengo kukidhi mahitaji ya wateja wake ili kwenda sanjari na sera ya Zanzibar ya uchumi wa Buluu.

“Benki yetu ni wadau wakuu wa Viwanda na wafanyabiashara wadogo wadogo hivyo ili kuboresha mustakabali wao tunalazimika kuwa na huduma bora zaidi kwa wateja na hata taasisi hususani za Kijamii,” amesema Duchi.

Pamoja na hayo, ameishukuru Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kwa kuandaa Tamasha hilo kwakuwa limetoa fursa kwao (NMB) kujifunza zaidi pamoja na kupata wigo mzuri wa kuonesha huduma zao.

Tamasha la Biashara la Saba la Zanzibar  lilikuwa na washiriki 360 lililofungwa Jumapili Januari 17, mwaka 2021 lilifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan Januari 6, mwaka 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles