26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania haibabaishwi, kawafundishe mabalozi wenzako- Rais Magufuli

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli amempongeza Balozi wa Uingereza nchini, David Concar, na kumtaka kwenda kuwafundisha mabalozi wenzake namna ya kuishi nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 18, mkoani Kagera kwenye hafla ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Ihungo baada ya kufanyiwa ukarabati upya.

“Ndiyo maana nawashukuru sana nchi wahisani kama Waingereza, Wachina ambao wamekuwa pamoja katika kulisukuma taifa letu katika maendeleo ya kweli na huu ndiyo undugu, na huu ndiyo urafiki wa kweli.

“Kwa hiyo mh balozi (David Concar) tangu umekuja nataka kukuthibitishia, umeimrisha sana mahusiano kati ya Tanzania na Uingereza sijakjusikia hata siku moja ukitweet wala, wewe unachapa kazi…haya ndiyo yanayotakiwa nah ii ndiyo kazi ya Balozi kujenga mahisianno na nchi yake.

“Kwa balozi na kupongeza ‘your too spesho congratulation’ kawafundishe mabalozi wenzako wajifunze namna ya kuishi vizuri na nchi ya Tanzania ambayo ni nchi ambayo haibabaishwi inafanyakazi kutokana na mishingi ya kimataifa.

Aidha, Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kumualika Waziri Mkuu wa Uingeraza, Boris Johnson kuja kutembelea nchini.

“Wewe ni mfano mzuri hongera…hongera…hongera sana na utakapozungumza na Uongozi wa Uingereza napenda kumualika Waziri Mkuu wa Uingereza ( Johnson) aje atembelee Tanzania na akija huku aje na misaada mingi zaidi ili mgeni aje mwenyeji apone,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles