27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wachimbaji watajwa kuwa hatarini kupata kifua kikuu

PASCHAL MALUL-KAHAMA

SERIKALI wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeshauriwa kuweka vituo vya afya vya upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu katika migodi midogo ya wachimbaji madini ya dhahabu kutokana na mazingira ya wachimbaji hao rahisi kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na wandishi wa habari meneja mradi wa kuthibiti kifua kikuu wilayani Kahama, uliochini ya shirika lisilo la kiserikali Shinyanga Development preventing HIV/AIDS (SHIDEPHA+), Erneus Mwinuka, alisema Serikali kwa kushirikiana na mashirika mengine inapaswa kuweka vituo vya upimaji ugonjwa huo katika migodi.

Alisema vituo hivyo vitasadia kubaini wagonjwa jambo litakalosaidia kuthibiti ugonjwa huo kwani kwa sasa imekuwa changamoto kwa watu hao kwenda kupima kwa kuogopa gharama.

Alisema wamekuwa wakisafiri kwenda katika migodi iliyopo wilayani humo na mwitikio umekuwa mkubwa kwa wachimbaji kujitokeza kupima hivyo ili kurahisisha huduma hiyo ni lazima kuwe na vituo katika migodi ili huduma iendelee kutolewa kila siku pamoja na elimu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Ofisa Mradi wa Kuthibiti Kifua Kikuu Halmashauri ya Mji wa Kahama, Annasia Mringo, alisema kwa mjibu wa takwimu za mradi huo, kuanzia Oktoba mwaka jana hadi April mwaka huu, watu 978 wamebainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo kati ya 59,000 waliopimwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles