26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kumbaka mtoto wake wa miaka 13

AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

MKAZI wa Mbezi Juu Said Rashid (36), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es salaam kwa shtaka la kumbaka mtoto wake.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu Anifa Mwingira, Wakili wa Serikali Matarasa Hamisi, alidai katika tarehe zisizojulikana kati ya Mwaka 2016 na Aprili 2019 eneo la Mbezi Juu, Wilaya ya Kinondoni mshtakiwa alimbaka mtoto wake (jina tunalo)mwenye umri wa miaka 13.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaotoa bondi ya Sh milioni moja kwa kila mdhamini.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yake itakaposomwa Juni 10 mwaka huu.

Wakati huo huo watu wawili Lucy Kulaba (41) na Sande Hassan (47) Wakazi wa Tandale, wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la kukutwa na pombe haramu ya gongo.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu Joyce Mushi, Mwendesha mashtaka wa Jamuhuri Ester Charles alidai Novemba 14 mwaka jana eneo la Tandale kwa Mtogole, Wilaya ya Kinondoni walikutwa na pombe haramu aina ya gongo lita 5.

Washatakiwa kwa pamoja walikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Washtakiwa wote walirudishwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana mpaka Juni 10, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles