MSANII chipukizi wa filamu nchini, Festo Kise ‘Kise’, anatarajia kuingiza sokoni filamu yake ya kwanza inayoitwa ‘Yatima Hadeki’ inayohusu mateso, misukosuko na mafunzo mbalimbali kwenye maisha ya Mtanzania.
Kise alisema hiyo ndiyo filamu yake ya kwanza kuiandaa na kucheza kama mhusika mkuu huku akitarajia kwamba italeta changamoto kwa wasanii wakubwa kutokana na maudhui ya hadithi yenyewe.
“Hii ni filamu yangu ya kwanza, naamini mashabiki wa filamu wataipokea vyema kwa sababu hadidhi yake ina mafunzo mbalimbali kwa jamii, itaongeza hamasa ya kufuatilia filamu za Tanzania kutokana na mafunzo yake,” alieleza.
Katika filamu hiyo pia wapo wasanii wenye majina makubwa nchini akiwemo Mzee Msisili, Swahib Suleiman na Barafu.