28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Shaa ashangazwa na wimbo wake wa ‘Toba’

shaaNA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA wa Bongo Fleva, Sara Kaisi ‘Shaa’, ameibuka na kudai kwamba anashangaa video yake ya wimbo wa ‘Toba’ kupokelewa vizuri na kwa haraka licha ya kurekodi wimbo huo miaka miwili iliyopita.

Akiuzungumzia wimbo huo, Shaa alisema kuwa wakati anaandika wimbo huo alilenga maisha ya miaka ya mbele ndiyo maana alipoutoa ukapata nafasi kubwa ya kuchezwa kwenye redio na runinga kubwa ikiwemo MTV Base.

“Sikutarajia kama ungefanya vizuri kwa sababu wimbo wenyewe umeandaliwa na prodyuza wa Nigeria, Big H miaka miwili iliyopita ambaye tuliwasiliana kupitia mitandao ya kijamii tukafanya kazi pamoja.

“Video nilipata wazo la kuifanya iwe katika mwonekano wa Kihindi nilipopeleka wazo langu kwa ‘director’ wa video yangu akamtumia mke wake wananikutanisha na kundi la wanenguaji wa asili ya Kihindi tukafanya video nzuri ambayo kwa sasa imeanza kufanya vizuri kupitia vituo mbalimbali vya redio na televisheni,” alifafanua Shaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles