25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate mjamzito?

JOKATE_MWEGELO4MWANAMITINDO Jokate Mwegelo, anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi miwili wa mwanamuziki, Ali Kiba anayedaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi ingawa mara kwa mara wamekuwa wakikana uhusiano huo.

Kwa mujibu wa mtandao wa kenyamoja taarifa za mrembo huyo mwenye haiba na mvuto kuwa na ujauzito wa miezi hiyo miwili zilianzia katika blog mbalimbali zinazomilikiwa na Watanzania.

Lakini wakati akizungumza katika mahojiano ya redio Clouds FM, Ali Kiba alisema hakutarajia mtoto na Jokate, huku akiongeza kwamba hakwenda kuzungumzia masuala ya uhusiano wake kwenye redio.

‘Siwezi kuzungumzia mahusiano yangu na si kweli natarajia kupata mtoto na Jokate,” aliandika katika mtandao wake wa kijamii.

Jokate alipoulizwa na MTANZANIA kuhusiana na ukweli wa ujauzito huo alishtuka na kudai kwamba yupo kwenye ‘shooting’ atafutwe muda mwingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles